HABARI MPYA

Waziri Mbarawa Afuta Mamlaka Za Maji 36

Katibu mkuu wizara ya Maji Profesa Kilila Mkumbo,amesema serikali imefuta mamlaka za maji safi na usafi wa mazingira 36 na sasa zitahudumiwa na mamlaka za makao makuu ya mikoa 25, zilizoundwa na kuongezewa majukumu ya utoaji huduma katika maeneo yake Hayo ameyasema jana jijini Dodoma wakati alipokuwa akitoa taarifa ya …

Read More »

Ofisi nyingine ya Kata yachomwa moto Morogoro.

Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Mlali wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na kuteketeza baadhi ya nyaraka za ofisi hiyo. Kufuatia tukio hilo mkuu wa mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro kuwatafuta na kuwakamata waliohusika …

Read More »

Serikali Yatoa Kauli Mahindi Kupanda Bei

Serikali imesema licha ya bei ya mahindi kuwa juu, haitaingilia kupunguza bei kwani ni nafasi ya wakulima kupata bei wanayotaka. Naibu Waziri wa Kilimo nchini Tanzania, Hussein Bashe ametangaza msimamo huo bungeni leo Jumatatu Novemba 11, 2019 wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Busega (CCM), Dk Rafael Chegeni. …

Read More »

Vilio na huzuni vyatawala tena mgodi wa Imalanguza Geita

Majonzi na huzuni vimetawala kwenye mgodi wa wachimbaji wadogo wa Imalanguza wilaya ya Geita kata ya Lwamgasa katika Kijiji cha Imalanguzu, mara baada ya kuwasili Naibu Waziri wa Madini Stanslausi Nyongo mgodini hapo akiwa na viongozi wengine waandamizi wa Wizara ya Madini, uongozi wa mkoa na viongozi wa dini kwa …

Read More »

Tangazo La Kuwarejesha Wagombea Wasio Na Makosa Ya Kikanuni Kwenye Uchaguzi Wa Serikali Za Mitaa 2019

Zoezi la Uchukuaji fomu, Urudishaji fomu, Uteuzi, Pingamizi na Rufaa lilianza tarehe 29/10/2019 na kumalizika tarehe 9/11/2019. Katika zoezi hilo jumla ya wananchi 555,036 kutoka Vyama mbalimbali vya Siasa walifanikiwa kuchukua fomu za kugombea. Na jumla ya wananchi 539,993 sawa na asilimia 97.3 walifanikiwa kurejesha fomu. Wagombea kutoka Chama cha …

Read More »