HABARI MPYA

DC Hanang aweka jiwe la Msingi Ukumbi wa Shule ya Sekondari BAMA

Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Ghaibu Lingo ameweka jiwe la Msingi katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Bama, unaoendelea kujengwa kwenye shule hiyo iliyopo Kijiji cha Lamay mkoani Manyara. Zaidi ya Shilingi Milioni 200 zinatarajiwa kutumika Mpaka kukamilika Kwa ukumbi huo ambao utakuwa unatumiwa na wanafunzi katika shughuli mbali mbali …

Read More »

Jamii yatakiwa kutibu maji kwa matumizi ya nyumbani

JAMII imetakiwa kipindi hiki cha masika ya mvua zinazoendelaea kunyesha kutibu maji kwa kutumia dawa zilizodhibitishwa na wizara ya Afya ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko. Ushauri huu umetolewa na Afisa Afya na mratibu wa uelimishaji Afya wa halmashauri ya mji wa Tarime,Agrey Hyera wakati akiongea na waandishi wa Habari …

Read More »

MAMEC WAGAWA MIPIRA KWA WAANDISHI MANYARA

WAANDISHI wa habari wa Mkoa wa Manyara, wametakiwa kujihusisha na michezo ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza kuliko kuandika habari za michezo bila kushiriki. Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Manyara (Mamec) Zacharia Mtigandi ameyasema hayo wakati akigawa mipira kwa waandishi wa habari wa klabu hiyo. Mtigandi amesema Mamec …

Read More »

MPAGAZE:Waandishi andikeni habari za kudumisha Amani nchini.

Waandishi wa habari wametakiwa kuandika habari za kudumisha Amani nchini na kuacha kupendelea kuandika habari za uchochezi na zenye kuleta taaruki. Wito huo umetolewa leo na Mwezeshaji wa mafunzo ya kujenga Amani hasa baada ya Uchaguzi Denis Mpagaze yaliyoandaliwa na mtandao wa redio za kijamii nchini (TADIO) Mpagaze amesema kuwa …

Read More »

Watoto wa Donald Trump Wawatupia Lawama wanachama wa Republican kwa ‘usaliti’ na Kutomuunga Mkono Baba Yao

WATOTO wawili wa kiume wa Rais Donald Trump wamewatupia lawama wanachama wa Republican kwa kutomuunga mkono baba yao anayekabiliwa na ushindani mkali kutetea mhula wa pili madarakani. Mtoto mkubwa waTrump, Don Jr amekikosoa chama hicho kwa kuwa “dhaifu”. Ndugu yake Eric ameonya: “Wapiga kura wetu hawatawahi kuwasahau mkijifanya wanyonge!” Hatua …

Read More »

Waangalizi wa Kimataifa: Madai ya Trump Hayana Msingi

Mkuu wa ujumbe wa waangalizi wa kimataifa kwenye uchaguzi wa Marekani amesema jana kwamba madai ya Rais Donald Trump hayana msingi, yanayosema kwamba kumefanyika udanganyifu katika uchaguzi huo. Michael Georg Link anayeongoza ujumbe wa Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE) ameongeza kuwa madai ya Trump yanadhoofisha imani ya …

Read More »