HABARI MPYA

Ndugai: Hakuna Kubebana…. Ukiwa Mbunge Bubu Umekwisha

Spika mteule wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amewataka wabunge waliochaguliwa na wananchi kutokaa kimya ndani ya Bunge kwani wananchi wamewachagua kwa ajili ya kuwasemea changamoto na kutafutiwa ufumbuzi. Akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Spika wa Bunge, Ndugai amesema, wabunge wanapaswa kujua walichokifuata ndani …

Read More »

Job Ndugai Achaguliwa Kuwa Spika wa Bunge juu

Job Ndugai amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Uchaguzi wa Spika, umefanyika leo Jumanne tarehe 10 Novemba 2020 bungeni jijini Dodoma katika Kikao cha kwanza, Mkutano wa kwanza wa Bunge la 12. Mkutano huo wa uchaguzi, umesimamiwa na Mwenyekiti wa muda, William Lukuvi …

Read More »

MANYARA: TAKUKURU YAMTAKA DUNGA KUREJESHA MILIONI 33 ZA WAKULIMA

MKURUGENZI wa kampuni ya Farm Green Implement (T) Ltd, Dunga Othman Omar ametakiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Manyara, kurudisha shilingi milioni 33.2 za wakulima wawili wa Wilayani Hanang’ alizochukua ili awanunulie matrekta mawili. Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Babati jana, Mkuu wa TAKUKURU …

Read More »

DAS SIMANJIRO: ZAWADI YA MTOTO NI ELIMU.

JAMII imetakiwa kutambua kuwa zawadi kubwa wanayotakiwa kutoa kwa watoto wao ni kuwapa elimu kwani itawanufaisha kwenye maisha yao ya baadaye. Katibu Tawala wa wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Zuwena Omary ameyasema hayo kwenye mahafali ya tisa ya shule ya awali na msingi New Light iliyopo Mji mdogo wa Mirerani. …

Read More »

BILIONI 66.8 KUTUMIKA UJENZI WA BARABARA YA TANGA HADI PANGANI

UJENZI wa kiwango cha lami wa barabara ya Tanga hadi Pangani yenye urefu wa kilomita 50 unatarajiwa kutumia bilioni 66.8 na utamalizika kwa kipindi cha miaka miwili. Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroad) Mkoa wa Tanga Mhandisi Alfred Ndumbaro alisema kwamba tayari mkandarasi alikwisha kupatikana wa kampuni kutoka nchini …

Read More »

Mbunge wa CHADEMA atoa ushauri kwa viongozi wake

Mbunge mteule wa jimbo la Nkasi Kaskazini, kupitia CHADEMA, Aida Khenani, amewataka viongozi wa chama chake kufuata sheria kama kuna maeneo wameona kuna dosari, lakini kwa upande wake hawezi kususia matokeo wala kukataa kuapishwa kwa ajili ya heshima ya wananchi wake waliomchagua. Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 9, 2020, …

Read More »