HABARI MPYA

Kamishna wa Maadili asema mwitikio wa matamko ya Mali za viongozi ni yakuridhisha, huku matamko 366 yakiwasilishwa kimakosa

Kamishna wa Maadili Harold Msekela, amesema kwa asilimia kubwa tayari viongozi wa Serikali tayari wameshawasilisha matamko yao, huku akibainisha kuwa bado kunauelewa mdogo kwa baadhi wa watumishi kuwasilisha matamko wakati hawakutakiwa. Akizungumza  na waandishi wa habari leo januari 9, 2020,  Nsekela amesema kuwa mawaziri, Manaibu waziri,Makatibu wakuu,viongozi wa vyombo vya …

Read More »

Vurugu zaibuka kwenye kikao cha kumjadili Meya DSM

Vurugu zimeibuka katika kikao cha Baraza la Madiwani wa jiji la Dar es salaam, wakati wa kikao maalum cha kujadili na kuamua hatma ya Meya wa jiji la DSM Isaya Mwita. Chanzo cha vurugu kimetajwa ni kusaini kwa mahudhurio kwa mtu ambaye hayupo ndani ya chumba mkutano, ambapo mtu huyo …

Read More »

Watahiniwa 333 wafutiwa matokeo

Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne na maarifa QT, kidato cha pili  na darasa la nne ambayo iliyofanyika mwezi Novemba mwaka jana,huku hilo  likifuta matokeo yote ya watahiniwa 333 waliofanya udanganyifu katika mtihani . Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji NECTA Charles Msonde …

Read More »

Serikali kuwawajibisha maafisa kilimo watakaoshindwa kusimamia kilimo

Serikali nchini imesema maafisa kilimo wanatakiwa kumsimamia na kumpa maelekezo mkulima ili kulima kilimo chenye tija,kutokana na wakulima wengi kutumia ardhi kubwa lakini matokeo yanayopatikana yamekuwa hayana tija. Waziri wa kilimo,ushirika na umwagiliaji Mh.Japhet Hasunga amesema serikali itawawajibisha maafisa kilimo endapo itabainika wakulima wanatumia ardhi kubwa katika kilimo bila ya …

Read More »

Mrema ameitaka Serikali ya Tanzania kumlipa bilioni 2

Mwenyekiti taifa wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema ameitaka Serikali ya Tanzania kumlipa Sh2 bilioni kama fidia ya kesi alizowahi  kusingiziwa chini ya Serikali ya awamu ya tatu ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa. Mbali na fidia pia amemuandikia barua Rais wa Tanzania, John Magufuli iliyo na malalamiko …

Read More »

Shambulio la Iran: Mafuta ghafi yapanda bei

Gharama za mafuta ghafi zimepanda kwa 1.4% kwa dola 69.21 za Marekani kwa pipa moja. Wakati huo huo gharama za mafuta kwenye soko la dunia zilishuka kutokana na mzozo wa Mashariki ya kati. Televisheni ya Taifa ya Iran ilisema kuwa shambulio lilikuwa ni kisasi baada ya kuuawa kwa kamanda wa …

Read More »

Rais wa ukraine atangaza Watu wote 176 kwenye ndege wamefariki

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema hakuna aliyenusurika katika ajali iliyotokea leo asubuhi baada ya Ndege ya Ukraine ‘ Boeing-737’ kuanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Ndege wa Imam Khomeini, Iran na kwamba Watu wote 176 waliokuwemo ndani ya Ndege hiyo wamefariki. “Nimesikitishwa na ajali hiyo na …

Read More »

Trump kutoa tamko dhidi ya shambulizi la iran

Kambi mbili za Jeshi la Marekani nchini Iraq zimeshambuliwa kwa makombora kadhaa huku Television ya kitaifa ya Iran ikitangaza kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya Qassem Soleimani aliyeuawa na Marekani katika shambulio la Drones Iraq. Rais Donald Trump amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo katika mbi zao …

Read More »