HABARI MPYA

Dkt. Mpango Acharuka: Aagiza Watumishi 22 TRA Wasimamishwe Kazi

WAZIRI wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, amemwagiza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Dkt. Edwin Mhede kuwasimamisha kazi watumishi 22 wa Mamlaka hiyo wakiwemo baadhi ya Maneja wa TRA wa Mikoa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili za kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kujihusha …

Read More »

Urambo yatoa mikopo ya milioni 167.2 kwa vikundi 27

HALMASHAURI ya Wilaya ya Urambo imetoa mikopo ya kiasi cha shilingi milioni 167.2 kwa vikundi 27 vya wajasiriamali toka Julai mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Baraka Zikatimu wakati akiwasilisha jana taarifa ya shughuli zilizofanyika katika kipindi cha kuanzia Julai hadi …

Read More »

Rais Magufuli Afanya Uteuzi mpya wa Naibu Waziri wa Madini

Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Shukrani E. Manya kuwa Naibu Waziri wa Madini. Prof. Manya pia ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kabla ya uteuzi huo, Prof. Manya alikuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania. Uteuzi …

Read More »

Watu watatu wafariki Uganda katika ghasia za uchaguzi

Polisi nchini Uganda imethibitisha vifo vya watu watatu kutokana na machafuko yaliyozuka alasiri ya Jumatano kufuatia habari za kukamatwa kwa mgombea urais Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine Machafuko hayo yalisambaa katika miji kadhaa na kusababisha watu wengi kujeruhiwa kutokana na risasi na mabomu ya kutoa machozi. Hii imewalazimu wagombea …

Read More »

Katibu Mkuu ANC anatafutwa kwa rushwa

Katibu Mkuu wa Chama Tawala nchini Afrika Kusini(ANC), Ace Magashule ambaye ni mtu maarufu ndani ya chama hicho anakabiliwa na waranti wa kukamatwa kwa madai ya rushwa. Madai hayo ni katika kesi ya kandarasi ya umma ya tangu alipokuwa Gavana wa jimbo la Free State nchini humo. Hii ni moja …

Read More »