HABARI MPYA

PICHA: Makamu Wa Rais Apiga Kura Sos Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika foleni ya kupiga kura kwa ajili ya kuchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani katika kituo cha SOS Mombasa Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu …

Read More »

Hussein Mwinyi na Maalim Seif wapiga kura Zanzibar

Wagombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Mwinyi na Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, tayari wamepiga kura hii leo visiwani humo, huku kila mmoja wao akiwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura. “Nawapongeza Wanzanzibar wote ambao wametumia haki yao ya kupiga kura na niwaombe …

Read More »

Hatuendi Kwenye Uchaguzi Kwa Jazba – Majaliwa

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasichague kiongozi kwa sababu ya jazba au hasira. Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Oktoba 26, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nalasi, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma katika mkutano uliofanyika kwenye …

Read More »

Buhari atoa wito amani huku jopo likianza uchunguzi wake

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa wito wa kudumishwa kwa amani huku jopo likianza kuchunguza unyanyasaji unaotekelezwa na polisi hii leo Jumatatu, uliotokea katika mji wa kibiashara wa Lagos. Jopo hilo la uchunguzi ni miongoni mwa mahitaji ya waandamanaji wanaotaka maafisa wa polisi watakaopatikana na makosa ya unyanyasaji wachukuliwe hatua …

Read More »

Matiko ajinadi kwa kutoa elimu ya mpiga kura

Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),Esther Matiko amewataka wapiga kura wenye sifa ya kupiga kujitokeza kwa wingi siku ya 10,28,2020.,ambayo ilipangwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kuwa siku ya kupiga kura. Matiko alisema jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyikia viwanja …

Read More »

Wasimamizi Wa Vituo Vya Kupigia Kura, Makarani Waongozaji Wapewa Mafunzo

Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu Jimbo la Busega Anderson Njiginya Kabuko, amewataka wasimamizi, wasimamizi wasaidizi na makarani waongozaji wa vituo vya kupigia kura katika uchaguzi mkuu kuzingatia maelekezo na mafunzo yote wanayopewa ili kufanikisha zoezi la Uchaguzi mkuu wa tarehe 28/10/2020. Kabuko ameyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo tarehe 24/10/2020 …

Read More »

Alichokisema Hussein Mwinyi akifunga kampeni Zanzibar

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Hussein Mwinyi amesema akipata ridhaa ya kuongoza ataboresha miundombinu ya umeme na kuwapunguzia gharama za nishati hiyo wananachi wasio na uwezo. Dk Mwinyi alisema hayo jana kwenye mkutano wake wa kufunga kampeni uliofanyika uwanja wa Demokrasia, Kibandamaiti Unguja mjini. Alisema dhamira …

Read More »