HABARI MPYA

Rwanda Yajiweka Kwenye Tahadhari Kubwa Kukabiliana na Nzige….Hadi sasa Wametafuna Hekta 70,000 za Mashamba Kenya, Somalia na Ethiopia

Rwanda iko kwenye tahadhari ya hali ya juu kufuatia uvamizi wa nzige unaoweza kutokea ambao kwa sasa wameonekana katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki, zikiwemo Ethiopia, Kenya na Somalia. Waziri wa kilimo na rasilimali ya wanyama wa Rwanda Bibi Geraldine Mukeshimana amesema, wizara yake iko tayari kukabiliana na uvamizi huo …

Read More »

Tahadhari Ya Mvua Kubwa na Upepo kwa Siku 5

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya mvua kubwa na upepo mkali katika baadhi ya maeneo ya Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dar es Salaam, Zanzibar na Pwani kwa muda wa siku tano kuanzia jana. Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, kuanzia jana hadi Jumapili, kunatarajiwa …

Read More »

7 Watiwa Mbaroni Kwa Kuwaua Kwa Mapanga Wanandoa Wawili

Watu saba wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera, wakituhumiwa kuwaua wanandoa wawili kwa kuwakata sehemu mbalimbali za miili yao, chanzo kikidaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi. Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa tukio hilo lilitokea Januari 14 mwaka huu saa saba usiku …

Read More »

Kesi Ya Kumuondoa Trump Madarakani: Maseneta 100 Waapishwa

Maseneta 100 wa Marekani wameapishwa Alhamisi kama baraza la mahakama litakaloshughulikia kesi inayomkabili Rais Donald Trump. Hakimu mkuu wa mahakama ya juu zaidi John Roberts aliapisha maseneta kuhakikisha wanatenda haki bila upendeleo. Wiki zijazo, maseneta wataamua iwapo Trump anastahili kuondolewa madarakani kwa makosa yaliyowasilishwa na Bunge la Wawakilishi. Kesi hiyo …

Read More »

Muda Wa Kusajili Laini Za Simu Hautaongezwa

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema serikali haitaongeza muda wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole, huku akitahadharisha kuwa katika siku zilizosalia, kasi ya wizi wa kimtandao kupitia simu za mkononi imeongezeka. Amesema hayo jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu siku …

Read More »

Mrisho gambo sina mpango wa kugombea ubunge….

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema hana Mpango wa kugombea Ubunge, tofauti na ambavyo imekuwa ikidhaniwa na baadhi ya Watu wakiwemo Wanasiasa wa Mkoa wa Arusha. Gambo amesema kazi ya kuleta maendeleo anayoifanya katika Mkoa wa Arusha, ni katika Utekelezaji wa kawaida wa majukumu aliyopewa na Mamlaka yake …

Read More »

Baba amuua mwanae wa miaka miwili kwa kumchoma na moto

Jeshi la polisi mkoani Kagera linamshikilia Juma Daniel, mkazi wa Kijiji cha Kazingati kata ya Keza wilayani Ngara, kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaa, mwenye umri wa miaka miwili. Daniel anadaiwa kumuuwa mwanaye huyo kwa kumchoma moto usoni na makalioni na kumjeruhi kwa kitu chenye ncha kali sehemu …

Read More »