Biden aanza kipindi cha mpito wakati Trump akikataa kukubali kushindwa

Biden aanza kipindi cha mpito wakati Trump akikataa kukubali kushindwa
Rais mteule wa Marekani Joe Biden amechukua hatua za kwanza kuelekea Ikulu katika siku 73, wakati Donald Trump kwa mara nyingine akikataa kukubali kushindwa na kujaribu kutilia shaka matokeo ya uchaguzi.

Huku salamu za pongezi zikimiminika kutroka kwa viongozi wa ulimwengu na wafuasi wakiendelea kusherehekea, Biden na makamu wa rais mteule Kamala Haris wamezindua tovuti ya utaratibu wa mpito, ya BuildBackBetter.com pamoja na akaunti ya Twitter ya @Transition46.

Tovuti hiyo ina vipaumbele vinne: Covid-19, kuufufua uchumi, usawa wa rangi na mabadiliko ya tabia nchi. Trump anapanga kuwasilisha msururu wa kesi mahakamani katika wiki ijayo kwa mujibu wa wakili wake Rudy Giuliani, ambaye alisema ana ushahidi mwingi wa kuwepo udanganyifu. Lakini Rais wa zamani Goerge W. Bush alisema “matokeo ni ya wazi” na akaongeza kuwa alimpigia simu “Rais mteule” Biden na Harris kuwapongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *