Benki ya CRDB yatoa msaada wa madawati 153 halmashauri ya Mbogwe mkoani Geita.

Benki ya CRDB imetoa msaada wa madawati 153 katika shule ya sekondari Masubwe wilayani mbogwe mkoani Geita ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa madawati 1942 katika shule za sekondari 16 zenye jumla ya wanafunzi 8,975.

Akipokea msada huo mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Martha Mkupasi ameishukuru benki ya CRDB kwa kuwapatia madawati hayo nakuongeza kuwa msaada huo umefika katika wakati sahihi.

Katika hatua nyingine Mkupasi amesema kuwa upatikanaji wa viti na meza hizo katika sekta ya elimu Wilayani Mbogwe utasaidia kuboresha mazingira ya kusomea kwa wanafunzi pamoja nayakufundishia kwa walimu hali itakayoinua kiwango cha Elimu wilayani humo.

Sambamba na hayo amewataka wanafunzi kuyatunza madawati hayo ili yadumu muda mrefu na kuweza kutumiwa na wanafunzi wengine wajao huku akitoa wito kwa wananchi wa Mbogwe kuendelea kutumia benki ya CRDB kufungua akaunti,Kuwema amana na kupata mikopo kwa riba nafuu.

Kwa upande wake meneja wa CRDB kanda ya Magharibi Said Pamui amesema kuwa viti na meza hizo zimegharimu shilingi milioni 9 laki 9 na elfu 45 na kuwataka wanafunzi na walimu kuyatunza ili yaweze kuleta tija sambamba na kupunguza tatizo hilo.

Benki ya CRDB kanda ya Magharibi inayojumuisha Mikoa ya Shinyanga,Tabora,Kigoma na Geita ina jumla ya matawi 24 huku mkoa wa Geita ukiwa na matawi 8 likiwemo na tawi la Mbogwe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *