BASHE:Vyama vya Ushirikia fufueni viwanda vya kuchakata Pamba kuepuka uuzaji holela wa pamba ghafi.

Serikali imewataka viongozi wa Vyama vikuu vya Ushirika nchini kuhakikisha wanavifufua  viwanda vya Kuchakata zao la Pamba vilivyoko katika maeneo yao ili kuondokana na uuzaji holela wa pamba ghafi inasababisha wakulimu kutonufaika na kilimo hicho.

Kauli hiyo imetolewa jana  Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe katika hafla ya Uzinduzi wa kiwanda cha kuchakata zao la Pamba kinachomilikiwa na  Chama kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) kwa ufadhili wa benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Alisema kuwa  KACU wamefanikiwa kufufua kiwanda hicho ambacho kilikuwa hakifanyi kazi tangu mwaka 2013 na kusaidia kutoa ajira zaidi ya 200 zilizorasimi huku kisaidia kuongeza tathamani ya zao hilo ambalo hapo awali wakulima walikuwa wanalazimika kuuza pamba ghafi kwa bei ya Chini.

“Tunataka faida za ushirika ziwanufaishe wakulima wa zao la pamba,tunawapongeza Viongozi wa KACU kwa kufufua kiwanda hiki hivi sasa mtakuwa mnauza pamba nyuzi kwa bei ya juu na tangu kuanza kufanya kazi kwake kumesaidia kupandisha bei ya zao hili kutoka shilingi 800 hadi 920,”alisema Bashe.

Aliongeza kuwa umefika wakati wa viongozi wa vyama vya Ushirika kufifufua viwanda hivi ili kuongeza ushindani katika masoko pamoja na kutoa ajira kwa Watanzania wengi zaidi kupitia uwepo wa viwanda hivyo ambavyo vitaleta tija katika ukuzaji wa uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alisema kuwa kiwanda hicho kimefufuliwa kutokana na viongozi wa KACU kuaanda andiko na kuliwasilisha katika benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB) ambayo waliwapatia mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 4 zilizosaidia kutengeza mitambo ya kiwanda hicho sambamba na kununua pamba za Wakulima.

Awali akisoma taarifa ya kiwanda hicho,Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika Kahama Emanuel Charahani alisema kuwa kiwanda hicho kiwesaidia kuongeza thamani mazao ya wakulima pamoja na kutoa ajira kwa watumishi zaidi ya 200 na kuiomba TADB kuwakopesha fedha kwaajili ya Ujenzi wa kiwanda cha kukamua mafuta ya Pamba.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alisema kuwa nia ya Serikali ni kuona thamani ya zao la pamba inaendelea kuongezeka ili kuwahamashisha wakulima kuongeza uzalishaji sambamba na kuandaa mpango mkakati wa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza nguo ambacho kitakuwa chini ya Usimamizi wa KACU.

“Niwaombe viongozi wa chuo kikuu cha Ushirika Moshi (MOCU) leteni wanafunzi wengi katika tawi la shinyanga ili kutoa fursa kwa wakulima kupatiwa elimu kuhusiana na umuhimu wa kujiunga na Ushirika sisi tupo tayari kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali zitakazo wakabili,”alisema Telack.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *