Balozi wa Uturuki mjini Paris asema kwamba kuna tofauti kubwa kati ya Ufaransa na Uturuki

Balozi wa Uturuki nchini Ufaransa Ismail Hakki  asema kwamba  Uturuki na Ufaransa ni mataifa washirika na rafiki na kusema kuwa    lawama dhidi ya Uturuki ni  kosa ambalo linaweza kutajwa kama kosa la kukusudia.

Balozi Ismail amesema kuwa huwa ikitokea kuwa na tofauti katika mitazamo  kati ya Uturuki  na Ufaransa.

Akiwa muarifiwa katika kituo cha redio cha Europe  1  balozi wa Uturuki mjini Paris amezungumza kuhusu  ushirikiano kati ya Uturuki na Ufaransa.

Katika  mahojiano hayo Ismail Hakki amesema kwamba lawama dhidi ya Uturuki hazina mashiko.

Balozi Hakki amekiri kwamba huwa kukitokea tofauti katika mitazamo kati ya Uturuki na Ufaransa licha ya kuwa ni mataifa washirika.

Balozi huyo amezungumza pia  kuhusu umuhimu  wa  gesi asilia  kugunduliwa katika  ukanda wa Bahari Nyeusi na hakuna uhasama kutoka Uturuki dhidi ya taifa lolote lile.

Ismail Hakki amezungumza pia kuhusu hali iliopo  Mediterania  Mashariki.

Ugiriki imeomba kuwa na udhibiti wa eneo kubwa katika bahari ya Mediterania jambo ambalo Uturuki ikiridhia italazimika kuomba ruhusa ya kuingia  katika eneo lake la majini  Ugiriki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *