Baba ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumchoma na pasi mwanaye

Moses Mwambene(35) Mkazi wa Mtaa wa Ilembo, Mbozi anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kumvua nguo na kumchoma kwa pasi Mwanae Victor Moses (12) na kumsababishia majeraha makali, tayari Polisi Mkoani Songwe wanamshikilia Moses.

“Kosa la kumchoma linadaiwa ni Baba alimzuia Mtoto kwenda kumsalimia Mama yake ambaye ametangana na Baba huyo baada ya kutokea ugomvi, lakini Mtoto akakaidi” – POLISI SONGWE

“Alimvua nguo akamuunguza kisha kumvalisha nguo na kumfungia ndani mpaka Majirani waliposhtuka, Madaktari wamepata shida kumvua nguo zimegandana na mwili”-POLISI SONGWE

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *