BAADA YA BIRIANI LA SIMBA KULIWA,NENO LAO HILI HAPA

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba baada ya kupotezwa na faslafa yao ya mpira biriani kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons Uwanja wa Nelson Mandela, nahodha msaidizi, Mohamed Hussein amesema kuwa ni sehemu ya matokeo.

Mchezo huo ulikuwa ni wa sita kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck huku ukiwa ni wa kwanza kwake kupoteza kwa msimu wa 2020/21.

Mechi tano za mwanzo alishinda mechi nne na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na jana pira biriani lilikwama mbele ya Prisons ambao walikomba lote na kusepa na pointi tatu mazima.

Ushindi huo unaifanya Simba ishushwe kutoka nafasi ya pili na watani zao Yanga ambao jana walishinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Uhuru.

Nahodha huyo amesema:-“Ni sehemu ya matokeo ya mchezo. Naamini mwalimu ameona makosa na tutaenda kuyafanyia kazi ili mchezo ujao turudi vizuri zaidi.”

Tanzania Prisons inafikisha jumla pointi tisa ikiwa imecheza mechi saba ipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Kinara ni Azam FC mwenye pointi 21 baada ya kucheza mechi saba msimu wa 2020/21.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *