Askofu wa Anglikana akemea wanasiasa wanatafuta madaraka kwa ushirikina

Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika (DCT), Dickson Chilingani amewataka Watanzania kuitumia sikukuu kuzaliwa kwa Yesu Kristo kama siku ya kutenda mema badala ya kugeuza kuwa siku ya kutenda machafuko.

Askofu Chilongani ametoa kauli hiyo leo Jumatano Desemba 25, 2019 wakati akihubiri kwenye ibada ya sikukuu ya Krismasi katika kanisa Kuu la Roho Mtakatifu jijini Dodoma ambapo amesema ibada njema ni ya watu wanaoyaishi mambo mema ambayo Kristo mwenyewe aliyaagiza.

Amesema amani ni sehemu ya maandiko ambayo hata Kristo mwenyewe aliagiza hivyo watu wakiituza amani watakuwa wanamcha na kumheshimu yeye aliyemwanzilishi wa amani lakini kinyume chake hali inaweza kuwa mbaya.

“Itunzeni amani, fanyeni mambo kwa kuwazia amani na jinsi mnavyoweza kuwa vielelezo katika kumcha Mungu, siku kama ya leo zinatukumbusha kudumisha amani hiyo badala ya kuigeuza kuwa ya machafuko yanayoweza kusababisha kutoweka kwa maana halisi ya Krismasi,” amesema Askofu Chilongani.

Amewataka Wakristo kuwa kielelezo katika kulinda amani hiyo ili watu wengine waweze kuiga matendo na mienendo yao kwa kuwa wengi hujifunza kupitia kwa watu wanaoingia kwenye nyumba za ibada.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *