Askari anayetuhumiwa kumpa ujauzito mtoto wa darasa la saba asakwa

Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linamtafuta askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani anayetuhumiwa kumpa ujauzito mtoto wa darasa la saba mwenye umri wa miaka 14 ambaye inasemekana ni mtoto wa polisi mwenzake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Salum Hamduni (pichani) amethibitisha kuwa polisi mkoani humo wanaendelea na jitihada za kumtafuta polisi huyo ambaye awali aliripotiwa kuwa amekamatwa.

Wiki iliyopita kamanda huyo alisema kuwa mtuhumiwa tayari anashikiliwa kwa ajili ya mahojiano, lakini baadae ilibainika kuwa mtuhumiwa huyo hakuwa mikononi mwa polisi kwani alitoroka. “Ni kweli hatujamkamata kwa sababu alitoroka,” amesema RPC Hamduni

Taarifa kutoka mkoani humo zinaeleza kuwa mtoto huyo alikutwa na ujauzito wa miezi mitatu, na pia mawasiliano yake ya simu na polisi huyo yanaonesha kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *