ARSENAL YAPINDUA MEZA KIBABE

ARSENAL imeanza kwa ushindi wa mabao 2-1 ndani ya kundi B kwenye mashindano ya Europa League baada ya kupindua meza kibabe wakitokea nyuma na kushinda mabao 2-1 dhidi ya Rapid Wien.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Allianz Stadion, Taxiarchis Fountas alianza kupachika bao la kwanza kwa Rapid Wien lililopinduliwa na David Luis dakika ya 70.

Bao la pili na la ushindi lilipachikwa na nahodha Pierre Emerick Aubameyang dakika ya 74 na kuifanya Arsenal kusepa na pointi tatu jumlajumla wakiwa ugenini.

Mikel Arteta Kocha Mkuu wa Arsenal amesema kuwa anafurahi kuona vijana wake wanashinda na kuwataka waongeze juhudi zaidi katika kuboresha viwango vyao.

“Ni furaha kuona timu inapata ushindi kwenye mechi ambazo zina ushindani, kikubwa kinachotakiwa ni kwa vijana kuongeza juhudi katika kusaka matokeo ndani ya uwanja,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *