Aliyetangaza kuna ugonjwa wa zika nilimfukuza kazi- Rais Magufuli

“Wakati tunaingia madarakani tuliambiwa Tanzania kuna ugonjwa unaitwa Zika, aliyetangaza na aliyetumiwa kutangaza nikamfukuza kazi, bahati mbaya ni Mgogo, baada ya kumfukuza kazi siku chache akateuliwa na waliomtuma akatangaze kuna Zika akapewa Ukurugenzi”-JPM

“Baada ya kumfukuza yule Mgogo aliyesema Tanzania kuna Zika na waliomtuma wakamteua kuwa Mkurugenzi, mpaka leo miaka karibu mitano hapajawahi kuwa na kesi ya Zika hapa Tanzania”-JPM

“Baada ya uzushi wa Zika kupita na nilipomfukuza kazi aliyesema kuna Zika,tukakaa baadaye tukaambiwa kuna Ebola, walijua wakisema tuna Ebola Watalii hawatokuja,tukasema sisi hatuna Ebola, wala Mjukuu au Hawara yake Ebola, na kweli hatujaona mgonjwa amekufa na Ebola Tanzania”-JPM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *