Aliyemuua mwanamuziki Radio, Kwenda jela miaka 14

Mahakama Kuu nchini Uganda imemuhukumu kifungo cha miaka 14 jela Bwana Godfrey Wamala maarufu Troy kwa kosa la kumuua mwanamuziki Moses Ssekibogo maarufu Mowzey Radio. Troy alipatikana na hatia hiyo siku ya Jumatatu ambapo mashtaka yake yalisomwa.

Radio alifariki Februari 1, 2018 baada ya kupigana na Troy wakiwa baa mwaka jana.

Radio alifariki katika hospitali ya Case Jijini Kampala ambako alikuwa amelazwa baada ya kuripotiwa kupigwa na Godfrey Wamala hadi kupoteza fahamu kwenye klabu ya Starehe ya De Bar, iliyopo Entebbe.
Jaji Jane Abodo aliyekuwa akiendesha kesi hiyo amesema Godfrey Wamala atatumikia miaka 13, miezi 3 na siku 4 baada ya kukaa mahabusu kwa mwaka 1.
Jaji amesema kuwa rufaa iko wazi kama Wamala atakuwa hajaridhika na uamuzi uliotolewa na Mahakama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *