Aliyekuwa Kocha wa Mtibwa Sugar aibukia Ihefu

Zuber Katwila baada ya jana Oktoba 18 kubwaga manyanga ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar ambacho alikuwa nacho kwa muda mrefu ametangazwa kuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Ihefu ya Mbeya.
Katwila anachukua mikoba ya Maka Mwalwisi aliyefutwa kazi Oktoba 6 ndani ya Ihefu FC kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo ambayo imepanda Ligi Kuu Bara msimu huu.

Wakati anasepa ndani ya Mtibwa Sugar, timu yake ya zamani ilikuwa kambini Morogoro ikijiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC ambao utachezwa leo Oktoba 19 Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mchezo wake wa mwisho Katwila kuiongoza timu yake ilikuwa ni dhidi Biashara United ya Mara ambapo Mtibwa Sugar ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.

Kwa sasa Mtibwa Sugar ipo chini ya kocha msaidizi Vincent Barnaba aliyekuwa akifanya kazi na Katwila.

Akiwa kwenye benchi kwenye mechi sita ambazo aliongoza aliambulia ushindi mchezo mmoja dhidi ya Ihefu FC kwa kuifunga bao 1-0 na alilazimisha sare mbili huku akipoteza mechi tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *