Afghanistan yawaachilia huru wafungwa 100 wa Taliban

Wafungwa 100 wa kundi la Taliban wameachiwa kutoka gereza la kijeshi nchini Afghanistan hii leo, kama sehemu ya jibu la serikali baada ya wanamgambo wa Taliban kutangaza usitishwaji vita kwa siku tatu kusherehekea Eid ul-Fitr.

Serikali ya Afghanistan inapanga kuwaachia huru hadi wafungwa 2,000 wa kundi la Taliban kama ishara ya nia njema, kufuatia tangazo hilo lao la jana na hivyo kuimarisha juhudi za kuanzisha mazungumzo ya amani.

Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Taliban na Marekani mwezi Februari yalisema serikali ya Afghanistan itawaachilia huru wafungwa 5,000 wa Taliban, nao wanamgambo hao watawaachilia maafisa 1,000 wa usalama wa serikali wanaowashikilia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *