ADAM ADAM AWEKA REKODI YAKE WAKATI JKT TANZANIA IKIITUNGUA MABAO 6-1 MWADUI

ADAM Adam mshambuliaji wa JKT Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu Abdalah Mohamed, ‘Bares’ leo Oktoba 25 ameibuka shujaa ndani ya timu hiyo wakati wakiitungua mabao 6-1 Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex.

Kwenye ushindi huo wa mabao sita, Adam amefunga jumla ya mabao matatu ikiwa ni hat trick ya kwanza ndani ya msimu wa 2020/21.

Mabao hayo aliwafunga dakika ya 24, 48 na 82 huku yale mengine mawili yalifungwa na Lyanga dakika ya 40 na 52 moja lilipachikwa na Luyaya dakika ya 90+2.

Bao la kufuta machozi kwa Mwadui lilipachikwa na Pastory Athanas dakika ya 60 na kuwafanya Mwadui waache pointi tatu zikisepa jumlajumla.

Hii inakuwa mechi ya kwanza kwa timu moja kufunga mabao mengi ambayo ni sita na pia mchezo wa leo umekusanya mabao mengi ambayo ni saba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *