Mvua kalii zilizonyesha nchini Brazil zimepelekea maporomoko ya ardhi ambayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.
Kiongozi wa kitengo kinachohusikana na usalama wa rais katika eneo la Minas Gerais amewatahadharisha wakazi wa maeneo tofauti na mvua kali ambazo zimeripotiwa kuendelea kunyesha.
Kwa ujumla watu 46 wamefariki nchini humo huku 9 wakiripotiwqa kufariki katika jimbo la Minas Gerais na 37 katika eneo la Espirito Santo.
Majumba zaidi ya 20 yamekwanda na maji na watu takribani 28 hawajulikani walipo.
Siku tatu za maombolezo zimetangazwa katika jimbo la Minas Gerais na katika miji mingine 47.