KOCHA YANGA APOKEA MESEJI NYINGI KABLA YA KUANZA KAZI

CEDRICK Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga ambaye ametua Bongo usiku wa kuamkia leo amesema kuwa anachohitaji ndani ya Yanga ni sapoti ili aweze kufikia malengo ambayo Yanga wanahitaji.

Kaze amekuja kuchukua mikoba ya Zltako Krmpotic ambaye alifutwa kazi Oktoba 3 na uongozi wa Yanga.Na ameweka bayana kuwa amekuwa akipokea meseji nyingi kutoka kwa mashabiki.

Kaze amesema:”Ninaweza kusema kuwa nimepata faraja kubwa sana kuwa kocha wa Yanga na wengi wamekuwa wakinipongeza katika hili na meseji nimepokea nyingi sana.

“Kikubwa ambacho ninaweza kusema ni kwamba nimekuja kufanya kazi na ninachohitaji ni kuona wengine wanasapoti kazi yangu katika hili.

“Yanga ni timu kubwa na ina mashabiki wengi hivyo kinachotakiwa kwa sasa ni kuangalia namna gani tutafikia mafanikio na malengo ambayo tumejiwekea,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *