Wanafunzi waombwa kushiriki kuzima moto Mlima Kilimanjaro

Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (CAWMSO) amewaomba wanafunzi waliopo chuoni kushiriki kikamilifu katika kuzima moto katika hifadhi ya Kilimanjaro.
Mamlaka za Hifadhi za Taifa ilisema sehemu ya msitu wa mlima Kilimanjaro ilianza kuungua tangu jana mchana na waliendelea juhudi za kuuzima.

Kwa kuwa moto bado unaendelea Mkuu ametaka kuongeza nguvu kwa kuwaomba wanafunzi hao kushiriki kuanzia leo ili kuudhibiti moto huo kwa haraka.

Wanafunzi wametakiwa kuvaa suruali ya kombati ya kijani na buti na tisheti za chuo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *