Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema kuwa muda wa Wabunge wake kukaa karantini kwa siku 14, umemalizika siku ya jana na kwamba leo Mei 15, 2020, wanatarajiwa kurejea Bungeni na kuendelea na shughuli zao kama kawaida.

Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama hicho John Mnyika, na kusema kuwa Wabunge wote waliotekeleza agizo la Mwenyekiti wa chama hicho Freema Mbowe, walizingatia kanuni na namna bora za kujikinga kupata maambukizi ya Virusi vya Corona.

“Wabunge wetu wote ambao walitekeleza makubaliano na uamuzi wa chama wa kujitenga kwa siku 14, leo watarejea Bungeni kuendelea na shughuli za kuwawakilisha wananchi, huku wakiendelea kuzingatia tahadhari zote za kujikinga na kuwakinga w.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *