Serikali wilayani kahama, imeridhishwa na juhudi za halmaushauri ya mji katika kuboresha miundo mbinu ya Shule.

Serikali wilayani Kahama mkoani Shinyanga imesema imeridhishwa na juhudi zinazofanywa na halmashauri ya mji wa Kahama katika kuboresha  miundombinu ya shule mpya ya Msingi Mayila iliyofunguliwa  mwaka huu  baada ya rais John Magufuli kuagiza ifunguliwa.

Akizungumza  baada ya kutembelea shuleni hapo, Mkuu  wa wilaya hiyo ANAMRINGI MACHA amesema   kasi ya kuboresha   miundombinu ya shule hiyo inakwenda vizuri kutokana na juhudi zinazofanywa na halmashauri hiyo.

MACHA ameitaka halmashauri hiyo kuhakikisha  madawati na mahitaji mengine muhimu wanayakamilisha ifikapo jumatatu  ya wiki ijaqyo ijayo na kwamba  eneo lote la shule liboreshwe kwa kujengwa miundombinu bora ikiwamo Barabara, mitaro pamoja na kuimarisha mipaka ya shule hiyo.

Afisa elimu wa shule za msingi katika halmashauri hiyo ALUKO LUKOLELA, amesema  miundombinu yote ipo katika hatua za mwisho   na kwamba hadi jumatatu ijayo kila kitu kitakuwa sawa na kuwataka wazazi kuona umuhimu wa kujitolea  kusaidia kuboresha miundombinu hiyo.

Kwa upande wake mhandisi wa halmashauri hiyo,  FRANK ANATORI amesema wameshawasiliana na  wakala wa  barabara za mjini na vijijini TARURA katika halmashauri hiyo  ili kuboresha miundombinu wakati wa kiangazi kwa kujenga barabara yenye mitaro mikubwa ya kupitisha maji.

Katika hatua nyingine Mhandishi ANATORI amesema kwa Sasa pia wanajenga vyumba vinne vya madarasa kupitia  shilingi milioni tano iliyotolewa na rais MAGUFULI novemba 27, mwaka jana  na fedha nyingine  takribani shilingi. Milioni nne ambayo ilitolewa na wadau pamoja na mbunge wa Jimbo la Kahama JUMANNE KISHIMBA.

Shule ya Msingi Mayila imejengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na halmashauri ya mji wa Kahama ambapo jumla ya vyumba  nane vya madarasa na ofisi mbili zimejengwa huku Ujenzi wa  choo ukiendelea na kwamba jumla ya wanafunzi wa darasa la awali na la kwanza 535 wameandikishwa kusoma shuleni hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *