Mrisho gambo sina mpango wa kugombea ubunge….

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema hana Mpango wa kugombea Ubunge, tofauti na ambavyo imekuwa ikidhaniwa na baadhi ya Watu wakiwemo Wanasiasa wa Mkoa wa Arusha.

Gambo amesema kazi ya kuleta maendeleo anayoifanya katika Mkoa wa Arusha, ni katika Utekelezaji wa kawaida wa majukumu aliyopewa na Mamlaka yake ya Uteuzi, ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hata hivyo amesema hatapuuza maombi ya Wazee, kama watamuomba kugombea Ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *