Mahakama moja nchini Kenya katika kaunti ya Nakuru imeamuru mtoto wa miaka 11 anayeshikiliwa kwa tuhuma za kumuua kaka yake arejeshwe katika mahabusu ya watoto mpaka pale upelelezi wa kesi yake utakapokamilika.

Uamuzi huo umetolewa na hakimu mkazi Bernard Mararo baada ya mtoto huyu kukamatwa na polisi.

Kwa mujibu wa ripoti za awali mtoto huyo anadaiwa kumchoma kisu kaka yake mara baada ya kutokea kwa mtafaruku huo baina yao.

Wazazi wa watoto hao walikuwa wamesafiri kwa ajili ya sikukuu za mwisho wa mwaka na wakati tukio linatokea watoto hao walikuwa chini ya uangalizi wa mjomba wao.

Mahakama inaangalia uwezekano wa kumshitaki mtoto huyo kwakuwa sheria za nchi hiyo haziruhusu mtoto chini ya umri wa miaka 12 kushitakiwa maamuzi kamili yatatolewa baada ya siku tatu.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano inadaiwa kuwa alitenda tukio hilo siku ya tarehe 31 mwezi Disemba mwaka 2019 nyumbani kwao baada ya kutokea mtafaruku baina yake na kaka yake ambaye alimtuma kwenda kuchaji simu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *